Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

Zanzibar Maridhawa



Watu wengi wanayachukulia mahekalu kama utajiri mkubwa wa enzi hizo, ni ushahidi wa matumizi makubwa na mitindo ya maisha ya kifahari ya watawala kwa nguvu za watawaliwa.

Wengine wanahisi kwamba majengo hayo ya kisasa ni utajiri wa kihistoria wa aina ya watu, vielelezo vya utamaduni vya hao waliyajenga na kwamba wanastahili heshima na hata kupongezwa.

Kwa maoni yoyote yale, inaonekana waziwazi kwamba katika historia nzima jamii nyingi zilifikia hatua ya maendeleo ambayo ilitokana na ubunifu wa mahekalu/ngome, Jamii ya Zanzibar ilikuwa mojawapo.


Ngome ya Dunga

Nyumbani kwa Mfalme wa mwisho wa washiraz, Mwinyi Mkuu

Kwa muda mfupi aliishi katika ngome hii iliyokuwa ndani kabisa ya kisiwa wakati masultan wapya walijenga ngome pembeni ya ufukwe. Alifariki mwaka 1865, mtoto wake wa pekee alikuwa mgonjwa na hakuishi muda mrefu. Kwa mtoto huyo ukoo uliishia hapo na Ngome iliachwa ianguke. Kati ya mwaka 1910 na 1914 baadhi ya machimbo yalionesha mabaki wa mifupa ya binadamu na seti ya ngoma za mbao za sherehe.

Hivi karibuni kuta nyingi za zamani zimerudishwa na sasa ngome hiyo inaweza kutembelewa kama kituo cha kihistoria kukiwa na msindikizaji kwa bei ndogo.


Ngome ya Mtoni.

Ngome ya asili ya Seyyid Said.

Ngome za zamani za Zanzibar hapo mwanzo zilikuwa katika miundo kwa ajili ya kuishi. Zilitawanyika katika vyumbavyumba vingi na mara nyingi ziliungana na majengo ya jirani.

Ngome hizi za familia ziliweza kuwa kubwa na ziliweza kuhifadhi watu wengi hata 1000. Miundo yao ilikuwa ni rahisi na ya moja kwa moja.

Ngome ya Mtoni ilielezewa na mtalii mmoja kama ifuatavyo:

Mlango wa Nyumba kubwa ulielekea kwenye kivaranda cha kuingilia na kisha katika sehemu ya kati ya nyumba ambayo ilikuwa ni chumba cha wageni kilichopambwa kwa vioo virefu. Vyumba vya kuishi vilikuwa ghorofani juu.

Mbele ya nyumba kulikuwa na mnara wa duara...Sehemu ya juu ya mnara ilitumika kama veranda na ilikuwa na kiwambaza cha konakona nyingi. Mnara umekewa paa lenye umbo la koni kama hema.


Beit el-Hukm

Nyumba ya Serikali

Ngome za zilizofuatia zilianza kuwa kwa ajili ya matumizi maalum, baadhi zilikuwa ofisi zaidi na si ajili ya kuishi. Beit el-Hukm ilikuwa mojawapo. Moja kwa moja karibu na Beit el-Sahel kwa upande mmoja na Nyumba ya Maajabu kwa upande mwingine. Majengo haya yaliungana na njia za miguu zilizoinuliwa juu na kusakafiwa...zifaazo kwa ofisi nzuri.

Ngome hii iliharibiwa katika vita ya mwaka 1896. Leo hii sehemu hiyo imechukuliwa na bustani na nyumba ndogo ambayo inafanya kazi kama ofisi ya Mamlaka ya Uhifadhi na Maendeleo ya Mji wa Mawe.


Beit el-Sahel

Ngome ya makazi ya jijini.

Mwanzoni ilikuwa jengo tu kubwa la mstatili, mnamo mwaka 1870 Uwanja wa Sultani wa kupendeza uliongezwa kwa upande wa magharibi. Jengo hili lilihifadhi zaidi wanawake kuliko wanaume na kwa sababu hiyo wakati fulani lilijulikana kama Harem

Ni hapo ambapo Seyyid Barghash alijenga umbo kubwa la mtumbwi kwa ajili ya kuhifadhi maji yaliyohitajiwa na wapangaji wengi wa jumba hili.

Sayyida Salme, Binti wa Zanzibar na Oman, alikuwa na hili la kusema kuhusu maisha katika Ngome hii.

Kuna mandhari nzuri ya bahari....Milango katika ghorofa ya juu, ambayo ilikuwa na vyumba vingi, ilielekea katika ukumbi mrefu na mpana wa ukubwa ambao sijawahi kuona wa kulinganisha nao. Dari inashikizwa kwa nguzo .... na nguzo hizi zinaunganishwa kwa ukuta mrefu, ambapo viti vinawekwa. Taa nyingi za rangi, zilizotundikwa katika dari, zikitoa mwanga wa kupendeza katika nyumba yote baada ya giza.

Kumbi zaonekana chini katika uwanja, zikiwa zimejaa kelele na nendarudi....Ngazi kubwa mbili tofautitofauti zikielekea kutoka ukumbi huu kwenda ghorofa ya kwanza. Makundi ya watu yanaendelea kwenda juu na chini ya ngazi hizi, na mkusanyiko mara nyingi ni mkubwa sana kiasi kwamba inachukua dakika kadhaa kabla ya mtu kupanda ngazi.

Ngome hii hasa iliharibiwa katika vita ya mwaka 1896 lakini kuta zilizobaki upande wa kaskazini, ziliunganishwa kwenye ngome iliyojengwa upya ambayo ilibadilishwa tena mwaka 1936.


Hiyo Ngome iliyobadilishwa ikawa nyumbani kwa Seyyid Khalifa mjini pembeni ya bandari ambaye alitawala kuanzia mwaka 1911 hadi 1960. Wakati wa utawala wake wa miaka mingi ilijulikana kama Ngome ya Sultan

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 jengo hili lilitumiwa kama makao makuu ya serikali lakini hivi sasa limekarabatiwa na kufunguliwa tena kwa ajili ya wageni/watalii likiwa kama jumba la makumbusho zuri sana. Hivi limepewa jina la

Makumbusho ya Ngome.


Beit el-Ras

Nyumba juu Rasi.

Kwa muda mrefu kilichobaki ni uzio huu wa Ngome hii ilikuwa Sehemu kubwa ya kaskazini iliyoinuiliwa. Hebu fikiria mandhari nzuri za bahari kutokea katika Ngome hii ambayo haikuwahi kumalizika.

...ilianzwa mwaka 1847 na Seyyid Said, wajenzi wa uajemi wakiwa wameajiriwa. Katika kifo chake hali kadhalika, jengo lilikuwa bado halijamalizwa....mrithi wake alikataa kuimalizia. Kuta za kushikilizia zilivunjwa na rundo la kifusi lilitumika pamoja katika ujenzi wa reli ya Bububu. Rundo ambalo bado linaweza kuonekana....


Ngome ya Marhubi

Ngome ya makazi, kaskazini ya Mji wa Mawe.

Hapa palikuwa ni nyumbani kwa Seyyid Said.

Madimbwi ya baridi bado yanatuamisha maji.

Miundo ya kutokeza duara inayoonesha hapa chini ni Mabafu ya Kiajemi yaliyojengwa nyuma ya Ngome.


Aina nyingine ya Ngome zinazofahamika Zanzibar zilikuwa ni Ngome za Mashambani.

Hizi zilikuwa ni kwa ajili ya kuepuka adha na taabu za jijini. Hizi pia zilijengwa katika maeneo yanaoaminika kuleta faida kiafya.

Ngome ya Kibweni

Ilikuwa ni mfano mzuri zaidi wa aina hii.

Iliyojengwa mwaka 1915 Ngome hii hapo awali iliitwa Beit el- Kassrusaada (Ngome ya Furaha) lakini jina hilo halikutumika na sasa inajulikana na wote kwa jina la kijiji karibu na mahali ilipokuwa, kaskazini ya yalipo mabaki ya Beit el-Ras.

Ngome hii ilitumika wakati wa mapinduzi. Chini yake ni picha inayoonekana mara chache ya chumba cha ndani.


Ngome ya Chukwani

Hapo zamani karibu na kijiji cha Fumba takribani kilomita 15 kusini ya mji wa Mawe. Ilionekana nyumba ya kuvutia katika pwani shwari wakati ilipokuwa ikikaribiwa kutokea upande wa ndani wa ardhi lakini nyuma ya nyumba kulikuwa na ardhi kubwa iliyotulia juu ya mwinuko pamoja na njia za miguu zilizoelekea baharini. Ngome hii ilitumiwa kama aina ya bafu la usafi mpaka ilipovunjwa. Nyumba ya Bafu la Ngome bado ipo lakini sehemu hiyo haiwezi kutembelewa.

Ngome hii ilihusishwa na utawala wa huyo Sultan maarufu, Seyyid Ali bin Hamoud. (1902 1911)


Mabaki kidogo ya iliyo sanifu

Ngome ya Chuini

Ilijengwa ili iwe na maji yanayotiririka katika kipindi kabla ya umeme, ilijengwa katika ufuko karibu na mkondo kaskazini maghaharibi ya Zanzibar.

"Ngome hiyo, ambayo ilijengwa mwaka 1872 na Seyyid Barghash ipo katika uwanda wa mto, uwanda wa gharama kujitengenezea uliojengwa na kwa lengo la kuweka jengo chini ili mtitiriko wa kutosha wa maji upatikane. Utaalamu uliotumika ilikuwa ni njia iliyofunikwa iliyowekwa kwenye mishikio mirefu ya chuma juu ya mkondo wa karibu, chini ambapo bahari ilikuja katika mkondo kwa nyuma. Jengo liliunguzwa na moto mwaka 1914 na hakuna sehemu za maana zilibakia isipokuwa safu ndefu ya mabafu ambamo mkondo wa maji ulipitia kuelekea baharini.

Chuini foundation c1904


Beit el-Amani

Jumba la Makumbusho ya Amani.

Lilijengwa chini ya uangalizi wa waingereza katika mtindo ambao umeitwa Mtindo wa Haja muundo huu unaonekana ni aina ya Ngome iliyobuniwa kwa matumizi fulani lakini haikutumika hivyo. Iliwekwa mara baada ya vita kama kumbukumbu kwa hao waliopotezwa katika mgogoro huo, hivi sasa inatumika kama jumba la makumbusho likiwa na kazi nyingi za sanaa za kuvutia za kizanzibari.


Ngome ya Watu

Hapo awali ilikuwa Makazi ya Waingereza, jengo hili linaonekana ni mfano mwingine wa mtindo wa ujenzi wa waingereza. Likiwa kusini ya kingo za jiji Ngome hii leo inatumika kama Makazi ya Rais kwa ajili ya kiongozi wa serikali.

Baadhi ya sura nyingi za kuvutia ziko nyuma ya jengo, ambazo kwa sasa haziwezi kutembelewa.


Kuna Ngome nyingine za kale Zanzibar ambazo historia yake imepotea kabisa kwetu. Wanafunzi/watafiti wa siku zijazo watatakiwa kutafuta habari zake. Baadhi ya hizi sehemu zinajumuisha:

  • Ngome iliyopo Chake Chake katika kisiwa cha Pemba.

  • Mabaki yaliyopo Chwaka na Pujini, pia Pemba.

  • Mabaki makubwa zaidi katika kisiwa cha Tumbatu, kaskazini magharibi ya pwani ya Unguja.


Mbali na kazi zake nyingine, ngome zote zilijengwa ili kuendeleza hadhi ya mtawala wa wakati huo. Mfano mmojawapo wa aina hii ya Zanzibari ikiwa maarufu.

Beit el-Ajaib

Pia lilijulikana kama Jumba la Maajabu.

Jumba la Maajabu halikuonesha muonekano huo wakati lilipojengwa kwa mara ya kwanza, lilionekana labda pana kidogo, katika nyakati hizo.

Hata hivyo uharibifu uliofanywa kwenye jengo hilo wakati wa vita ya mwaka 1896 ulifanya lihitaji ukarabati mkubwa na tangu mnara wa saa katika nyumba ya kuongozea meli mbele ya Ngome/Jumba hilo ulipoharibiwa katika vita hiyo, iliamriwa kuunganisha miradi na kuweka mnara wa saa mpya kipindi cha kukarabati wa ngome.

Matokeo kwa kweli yalikuwa ni jengo kubwa ambalo kwa sasa lina umri wa miaka 100.



Imekusanywa na kuhaririwa mwaka 2003 na

Barghash@msn.com

Mahsusi kwa kumbukumbu ya mama yangu

Upendo wake kwa ajili ya Zanzibar ulizidishwa hasa na upendo kwa ajili ya familia yake.

Haki zote zimehifadhiwa.

Hit Counter

Imetafsiriwa na Mwalimu George Mwidima gmwidima@yahoo.com

Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI