Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

Michoro ya Kale ya Zanzibar

Michoro ya W. A. Churchill.

William A. Churchill alikuwa jamaa mdogo wa Baraza la Ushauri la Waingereza hapo Zanzibar mwishoni mwa miaka ya 1860's. Alikuja kwa ajili ya ziara visiwani akileta kipaji chake tu na ubao wake wa kuchorea lakini hivi vilifanikisha mwonekano fulani mzuri wa Zanzibar ya kale.


Reli ilioneshwa katika mchoro huu mzuri sio ile reli maarufu ya Bububu, ambayo ilijengwa mwaka 1905 na ikaelekea kaskazini nje ya mji baada ya kupitia karibu na N'Gambo. Kwa kiasi fulani ni reli ya zamani sana ambayo ilijengwa na Sultan Barghash.

Hii reli ya kipimo chembamba ilikuwa ni moja ya njia za mwanzo zilizotandazwa katika Afrika ya kusini mwa Jangwa la Sahara. Ilielekea kusini ya mji kwenye Ngome ya Sultan ya Chukwani. Mabehewa hapo mwanzoni yalivutwa na farasi wakati reli ilipofunguliwa lakini mwaka 1881 injini ya kiberenge cha kwanza iliyowahi kuingizwa Afrika Mashariki iliwasili kutokea Uingereza. Kiberenge hiki kiliitwa "Sultanee" na kilivuta mabehewa katika reli hadi kilipofungwa/simamishwa mwaka 1892.

Katika mchoro huu Churchill aliweka picha ya mmoja wa wafanyabiashara wengi kutoka dunia nzima ambaye alichukua makazi katika Zanzibar ya zamani.

Jeshi la Zanzibar halikuwa limewekwa vizuri nyakati zile, Jeshi la Majini likiwa na kipau mbele zaidi kwenye vifaa bora na watu, lakini bado taratibu zake za kuajiri za waziwazi zilisababisha jeshi kuwa angalau sehemu ya muda mfupi ya wanajeshi wengi wataalamu wa umri huo.

Hata wanawake walifanya asilimia kubwa ya nguvukazi ambayo iliufanya Mji Mkongwe uendelee mbele kama jiji lifanyalo kazi lililotulia kwenye kingo za nyika kubwa na kwa wakati huo sehemu kubwa ya nyika ya bara haikuwa imejulikana ambayo ilikuwa Afrika ya zamani.

Baadhi ya wanawake wa Zanzibar wanaoneshwa kama ni watu wenye nguvu katika jamii.

Miundo ya Serikali ilivutia Umakini wa Churchill.

Kama ambavyo alivyovutwa na matatizo ya watumwa na roho za majeshi ya Sultan.

Kabla ya mwishoni mwa miaka ya 1800's Livingston alionekana kama shujaa na mjitoa mhanga nchini Uingereza.

Hili chapisho zuri lazima lingeuzwa sana.


Churchill alitumia ufundi fulani wa kisanii katika michoro yake (akionesha labda bidii ya Mzoefu) lakini bado kazi zake nyingi zilikuwa za maisha ya kweli hasa. Hapa chini ni baadhi ya picha za zamani za matukio kama hayo ambayo lazima yatakuwa yamemwongoza katika michoro hii.


Ndugu wa W. A. Churchill alikuwa mwanadiplomasia bwana Henry Adrian Churchill ambaye alikuwa mshauri wa Baraza la Zanzibar tokea mwaka 1867 hadi mwaka 1870. H. A. Churchill alikuwa na kazi ya Udiplomasia kwa muda mrefu, alionekana kuvutiwa katika kusaidia watu popote alipofanya kazi, aliandika makala kuhusu kipindupindu hapo Zanzibar mnamo mwaka 1870, akiwasiliana na wanasayansi kuhusu uwezekano wa matumizi ya ndege fulani wa kichina ili kupunguza makundi ya mbung'o wa bara na alifanya kazi kama mkufunzi kwa ajili ya mtu maarufu zaidi wa Baraza la Ushauri la Uingereza John Kirk, ambaye alimtumikia kama daktari wa upasuaji na mshauri wake msaidizi miaka hiyo.

Kabla ya kuteuliwa kwake Zanzibar Churchill mkubwa alifanya kazi kama katibu na mkalimani kwa wafanyakazi wa Kamishna/Mwakilishi wa Uingereza, akiwa na Jeshi la Uturuki barani Asia, alishiriki katika ulinzi wa Kars, na alikuwa kwa muda mfungwa wa Urusi. Nafasi yake ya mwisho alikuwa Mshauri wa Uingereza huko Palermo mwaka 1879. Alifariki mwaka 1886.

Kidogo si dhahiri/wazi ni lini William alimtembelea kaka yake Zanzibar na uchelewashaji mkubwa katika uchapishaji wa hii michoro ambayo haikuwekea sahihi wala tarehe, (haikuchapishwa hadi mwishoni mwa miaka ya 1800's) yote haya yanaifanya kazi ya kuiwekea tarehe michoro hii iwe ngumu. Mbali na hayo, tukichukulia kuwa William hakukaa sana Zanzibar baada ya kuondoka kwa ndugu yake kutokana na afya mbaya, basi naamini hizi ni mandhari za Zanzibar kuanzia takribani mwaka 1870.



Imekusanywa na kuhaririwa na Barghash 2004.

Haki Zote Zimehifadhiwa.

Barghash@msn.com

Imetafsiriwa na George Mwidima

gmwidima@yahoo.com

Up Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI