Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

KITUO CHA ANGA ZANZIBAR


Kiasi cha kilomita 15 mashariki ya Mji Mkongwe, karibu ya kijiji cha Tunguu, yapo mabaki yaliyochakaa ya kituo cha Rada cha Kimarekani. Kituo hiki kilijengwa mwaka 1960 kwa ajili ya kunasia na kuwasiliana na misheni ya mwanzo ya kimarekani ya kwenda angani. Kituo hichi kilitumika kwa mara ya mwanzo wakati mradi wa mwanzo wa kwenda kwenye Sayari na "Mercury" ulipoanzishwa wakati wanaanga waliporuka katika Parabola yao kutoka Florida kwenda upande mwingine wa Afrika. Kituo hiki vile vile kipo mlalo wa njia ya dunia" Earth track" ya misheni za baadae za mzunguko kwenda kwenye Sayari na kwa hivyo kilikuwa kituo muhimu cha kunasia na pia cha upimaji na upitishaji wa data ambacho kilisaidia kuwasiliana na vyombo hivi vya Angani.

Kituo hiki kilifungwa mara tu baada ya Mapinduzi ya 1964. Serikali mpya ya Mapinduzi ilidai kwamba Rada za kituo hich zingelitumika kuelekezea makombora Zanzibar. Wafanyakazi wa kituo hiki walihamishwa kwa haraka wakati huo chombo cha jeshi la wanamaji cha kimarekani (U.S Navy Destroyer) kilikuwa mbali kidogo na Mji Mkongwe kuhakikisha kwamba mafundi sanifu wa kimarekani na familia zao wanaondoka bila ya kusumbuliwa.

Kwa leo ni tabu sana kugundua wapi kituo hiki kilikuwepo, lakini ikiwa utaelekea kusini kidogo ya njia kutoka Mji Mkongwe kuelekea mwambao wa Mashariki, kabla kidogo ya kufika Tunguu, mara tu utashtukia njia isiyoyakawaida iliyokaa sawa inayoongoza kuelekea kule ambako bado wenyeji za zamani wanaita majengo ya Wamarekani. "The Americani Buildings". Bora ya majengo haya yaliyohifadhiwa ni jengo la matengenezo la Mhudumu Mkuu (Butler - Aluminium Building) ambalo bado lina jenereta la dizeli ambalo lilikuwa linatumika kuendeshea kituo hiki cha Anga. Vile vile, karibu yake lipo Bweni (Dormitory building) ambalo lilikuwa linatumika na mafundi sanifu tu wakati misheni inatekelezwa. Wakati mwingine wamarekani hawa wote na familia zao waliishi karibu au ndani ya Mji Mkongwe ikiwa ni mchanganyiko wa jamii ndogo katika Zanzibar yenye mchanganyiko wa watu kutoka sehemu tofuati za dunia.


Jewels Pemba The Green Isle Southern Pemba & Mesali Isle

Unguja Island showing the east coast

Unguja; showing Zbar City Peninsula and and Harbor Reefs


Up Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI