Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

Kupiga mbizi zanzibar


Maji ya Bahari ya Azania yanachangia katika kupatikana kwa maarifa mazuri ya kuogelea, kupiga mbizi na kuzamia duniani. Yapo makampuni mengi katika mji mkongwe yanayojishughulisha na upigaji mbizi na baadhi yako katika fukwe ndefu za kitalii. Zote hizi hutoa huduma za upigaji mbizi na zinaweza kutayarisha safari za kupiga mbizi katika miamba ya karibuni na katika visiwa vidogo vidogo. Kituo cha Taifa cha mambo ya Baharini kilifunguliwa karibuni huko kisiwa cha Chumbe, maili 12 tu kusini Magharibi mwa mji mkongwe. Huko kuna miamba ya matumbawe mizuri na aina mbali mbali za viumbe vya kushangaza vya baharini na pia fursa ya kupiga mbizi na kuzamia hupatikana sambamba. Boti za kukodi vile vile huondoka mji mkongwe kuwapeleka wapiga mbizi katika kisiwa cha Pemba. Huko utaweza kuona kwa macho yako wakati unapiga mbizi katika maji meupe ya uvuguvugu (maji ambayo jicho linaweza kuona chini kati ya futi 60 hadi 2000), nje ya Kisiwa cha Mesali, ambako utaweza kupata maana halisi ya msemo "furaha ya kina".

Ifuatayo hapa ni orodha ya baadhi tu ya visiwa vidogo vidogo, miamba, fungu za mchanga na visiwa vya matumbawe vinavyofaa kwa kupiga mbizi kote Unguja na Pemba. Hadhi au daraja za uzuri wa sehemu hizo zimo katika kitabu kipya (1997) cha Anton Koornhof kiitwacho "Maeneo ya kupiga mbizi Kenya na Tanzania" (kilichochapishwa na Passport Books, Chicago 111 USA).


Maeneo ya Kupiga Mbizi Karibu Mji Mkongwe

Kisiwa cha Changuu (Prison Island) ni kizuri kwa kuzamia kwa kutumia vifaa vya hewa. Ni sehemu iliyo mita 35 tu Kaskazini Magharibi ya ufukwe.

Kisiwa cha Chapwani (Grave Island) = Ni kizuri pia kwa kuzamia, mita 50 Kaskazini Magharibi kwenye ncha ya Kaskazini ya kisiwa.

Kisiwa cha Bawe: Koornhof amekipa hadhi ya 4 kwa kupiga mbizi na kwa kuzamia. Ukuta wa mwamba upo umbali wa mita kama 150 Kaskazini mwa ncha ya Kaskazini ya kisiwa.

Fungu Chawamba (Sand Bar) = kipo umbali wa kilomita 3 Magharibi ya mji mkongwe. Kampuni nyingi za upigaji mbizi za mjji mkongwe hulitumia fungu hili kwa wale wanaoanza kuogelea kwa kutumia chupa za hewa.

Nyange (eneo ambalo halikuwekwa maboya) Koornhof amelipa sehemu hii hadhi ya kwanza kupiga mbizi na kwa kuzamia.

Kisiwa cha Pange - Kornhof ameipa sehemu hii hadhi ya kupiga mbizi na kuzamia.

Kisiwa cha Pwaku = Koornhof ameipa sehemuhii hadhi ya kupiga mbizi na kuzamia.

Kisiwa cha Murogo: Koornhof anakipa kisiwa hiki hadhi ya kupiga mbizi na kwa kuzamia.

Fungu mchanga la Boribu (vile vile linaitwa Bokibu) Koornhof analipa hadhi ya kupiga kupiga mbizi na kwa kuzamia.

Kisiwa cha Chumbe: Kibali kinahitajika kwa wale wanaokwenda kupiga mbizi kwenye hifadhi ya Maisha ya Baharini lakini pesa zinazotozwa ni muafaka na kinatilia mkazo mwamko wa mazingira. Katika kisiwa hiki upo mnara maarufu.


Maeneo mengine ya kupiga mbizi Unguja

Stringray Alley: hutumika kwa kupiga mbizi na haifai kuzamia. Sehemu hii ipo mwambao wa Mashariki ya Unguja, Mashariki ya Shehe Guest House, karibu na kijiji cha Jambiani.

Mwamba wa Jambiani: (vile vile panaitwa Mwamba wa Pembe moja) Hutumika kwa Kupiga mbizi na hapafai kwa kuzamia. Upo dakika 30 tu Mashariki ya kijiji cha Jambiani kwa kutumia mitumbwi ya kienyeji.

Levan Bank: Hutumika kwa kupiga mbizi na hapafai kwa kuzamia. Sehemu hii ipo nje ya kijiji cha Nungwi, kwenye ncha ya Kaskazini mwa kisiwa kikuu.

Kisiwa cha Mnemba Hutumika kwa kupiga mbizi na kuzamia. Hiki ni "kisiwa binafsi " nje ya mwambao wa Kaskazini Mashariki.


Maeneo ya Kupiga Mbizi Pemba.

Kisiwa cha Mesali: Kisiwa hiki kinanipendeza binafsi! Vile vile kinaitwa kisiwa cha Nahodha Kidd na kinaaminiwa kuwa bado kuna hazina yake iliyofukiwa . Kipo upande wa Magharibi ya mji wa Chake chake. Hadhi yake ni kupiga mbizi na kuzamia. Kinastahiki kabisa hadhi hiyo.

Kipengo cha Uvinje: Zipo sehemu mbili za kupiga mbizi katika sehemu hii ya Kaskazini Mashariki ya Chake. "Ukuta wa Kaskazini" umepewa hadhi ya kupiga mbizi lakini hapafai kuzamia, wakati "Ukuta wa Kusini" una hadhi ya kupiga mbizi na kuzamia.

Kisiwa Panza: Kipo karibu na ncha ya Kusini ya kisiwa cha Pemba. Sehemu hii ina maeneo mawili pia. Eneo la kwanza linaitwa "meli ya kusini," karibu na meli ya mizigo iliyozama, ambapo pana hadhi ya kupiga mbizi na hapafai kwa kuzamia. Kusini kwa meli hiyo iliyozama upo "mwamba wa zumadiri penye hadhi ya kupiga mbizi na pia hapafai kwa kuzamia.


Ncha ya Taa:

Hii ipo nje ya mwambao wa Kaskazini Magharibi ya Pemba, karibuna kisiwa cha Fundo.

Hapa pana hadhi ya lakini hapafai kuzamia. Sehemu hii inajulikana hivyo kwa sababu ya idadi kubwa sana ya taa, wakubwa wa taa ufukweni mwa kisiwa cha Pemba mara nyengine hutumika kama eneo ka kupiga kambi kwa vikundi vya wapiga mbizi.


Anuani kwa Wapiga Mbizi

One Ocean Zanzibar Diving Centre: Moja ya kampuni nzuri ya wapiga mbizi zanzibar na kupiga mbizi popote kwa kutumia madau.

http://www.webworks.com.

au/zanzibar/zdcmain.htm

Dive Africa Water Sports : imeunganishwa na ramani ya mawasiliano ya upigaji mbizi kaskazini ya unguja.

http://www.diveafrica.com/zanzibar/index.html

Rising SUN dive Centre : kampuni ya kupiga mbizi mwambao wa mashariki.

http://www.risingsun-zanzibar.com/main.html

Bondei Travel : Utaratibu wa biashara ya kupiga mbizi na orodha ya bei.

http://www.bondei-travel.dk/DIVING.htm#Mafia%20Island

UV-bilder frn Zanzibar-1998 =Kuna picha nyingi nzuri za ndani ya maji.

http://www.eminds.se/ka/uv/Zanzibar-1998/

New Africa Com = Ramani nzuri iliyounganishwa na mawasiliano ya upigaji mbizi katika kisiwa Mafia.

http://www.newafrica.com/travel/mafia/

New Africa.com = kisiwa chengine kizuri cha kupiga mbizi katika kisiwa cha Pemba

http://www.newafrica.com/travel/pemba/

Chumbe Isle Home page = Kupiga mbizi katika hifadhi za matumbawe

http://www.xtra-micro.com/work/chumbe


Habari nyengine kwa wapiga mbizi.

Joto la maji katika sehemu zote ni kati ya nyuzi joto 25 hadi 29 kwa kipimo cha senti grade.

Hali ya usafi wa bahari mtu anaweza kuona chini ya maji kati ya mita 15 - 60. Kwa kawaida ni vizuri kwa wapiga mbizi kufanya hivyo wakati maji yanapoaanza kujaa, kwani wakati wa maji kupwa kunaweza kutibua bahari na kumfanya mtu asione chini.

"Msimu wa kupiga Mbizi" kuanzia Septemba hadi Machi lakini ukweli ni kuwa maeneo mazuri ya kupiga mbizi yapo kwa kipindi chote cha mwaka. Ni kinyume na sheria kwa wapiga mbizi kuvua kwa kutumia bunduki ingawaje wenyeji wamekuwa wakifanya hivo kama kawaida . Sehemu ya karibu za huduma za kupiga mbizi ipo Mombasa Kenya kwenye kituo cha wanamaji.


Kupiga Mbizi Usiku .

Kama unataka msisimko wa aina yake jaribu kupiga mbizi usiku katika moja ya maeneo ya yenye maji ya kina kifupi toka orodha ya sehemu zilizotajwa. Maji safi pamoja na kundi kubwa la viumbe vya baharini vyenye kutoa mwanga hufanya mandhari yaonekane ya kusisimua sana. Mara moja nilikuwa ninazaniwa kando ya kisiwa cha changuu wakati wa mwezi mpevu na niliyoyaona hapo hayawezi kusahaulika na katika usiku wa giza na kama utabahatika kupata maji muafaka unaweza kuona naonesho hata bila ya kuigia majini. Adrian Conan Doyle alitumia sehemu ya malipo ya babu yake ya uandishi vitabu kwa kuja kwenye maji ya aina hiyo katika m,iaka ya 1950. Haya hapa ni maelezo yake ya usiku mmoja alipokuwa ametia nanga katika dimbwi la maji lililotenganishwa na fungu, kusini mwa kisiwa cha Unguja.

"Taa za Mauti"

Huku tukiwa tuko kimya kabisa, tulisimama kuangalia. Ilielekea kuwa kulikuwa na anga kubwa la mwangaza lililotokea chini kabisa ya bahari, na kadiri lilivyokuwa linakaribia, liliifanya sehemu yote ya chini ya meli, mle mlimofikia maji, kuanzia kung'ara . Mwanga ule unapita moja kwa moja chini ya mkuku wa meli, wakati mimi nikiwa deki nimeshikilia chubwi ya risasi, nikairembea majini. Ghafla kundi lote lile likatawanyika na kugeuka ndimi moto wa kibuluu zinazofukuzana mithili ya vimondo gizani ndani ya maji. Lilikuwa kundi la samaki wakubwa. Kule! Alipiga kelele Anna. Na kule vile vile! Oh! Yalikuwa mandhari mzuri kabisa. Makundi ya samaki yalianza kutembea kama mkondo kutoka ndani ya dimbwi lile; huku wakitoa mwangaza hafifu kutoka umbali wa yadi mia moja, hivi, na taratibu wakawa wameunda vikundi vizuri vya rangi za buluu na kijani kuelekea baharini. Kwa kuwaangalia kwa makini sana , mtu aliweza kumaizi kuomba anga zile za mwangaza uliokuwa unatembea zilisababishwa na kundi zima la samaki wa ukubwa wa kadiri.

Saa zilipita na baada ya muda mrefu Anna aliondoka kwenda kupumzika. Makundi yale ya samaki yaliyokuwa yanatembea sasa yalikwishapungua sana nami nilikuwa tayari kuteremka wakati ghafla, nyuma ya Omo, lilichomoza anga jengine la mwangaza kwa mbali chini ya bahari. Lilikuwa linakuja karibu karibu zaidi na sasa nikawa naweza kuhesabu si zaidi ya makundi matatu yaliyofuatana moja nyuma ya jengine katika mstari mmoja mkubwa, huku yanatoa mwangaza wa kijani.

Samaki wale wakapita sambamba na meli, huku muundo sawa na umbo la almasi ukitoa mwangaza wa buluu, na mapezi yao yakiwa na ukubwa wa zaidi ya futi thalathini kutoka ncha hadi ncha. Walikuwa wakielekea gizani na kuwacha mkondo wa mwangaza usio na moto utadhani mahema makubwa yaliyokuwa yakiserereka. Hivyo ndiyo taa hao walivyokuwa wanapita.


Na Barghash 2001 Barghash@msn.com

Up Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI