Bustani za Victoria

Bustani hizi zilibuniwa na kupandwa na wataalamu wa kiGoa na zilitolewa kwa jiji na Seyyid Hamoud mwaka 1899. Zilizopo karibu na njia kuu kuelekea jijini bustani hizo zilitumika kama sehemu ya kukutania na kupumzika ya watu wa daraja la juu.