Mwanamke wa Zanzibar

Huu mkusanyiko wa kanga wa kuvutia mapema (karibu ya mwaka 1890) wasaidia kueleza kwanini uvaaji wa Kanga ulikuwa unapendwa sana wakati zilipoingizwa kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki.

Waarabu #7

Picha hii ya familia kutokea mwaka 1900 ya mtu, watoto wake wawili wa kiume na watumishi wawili haitambuliki.

Msichana wa Ngazija

Jamii ya Ngazija ilikuwa ni jamii ya watu wachache muhimu katika Zanzibar ya zamani.

Mtaa wa Soko la Samaki

Hapo Zanzibar uvuvi sikuzote umekuwa sehemu muhimu ya maisha. kila mji una mtaa wa soko la samaki.

Majahazi

Majahazi ya mwanzo yalitengezwa bila misumari wala scrubu. Badala yake hizi boti za mbao zilifungwa na kushonwa pamoja.

Mtaa wa N'Gambo

Sehemu ya N'gombo ya jiji la Zanzibar imeendelezwa tena na tena mara kadhaa katika historia yake.

Seyyid Hamoud

Katika hii picha ya mwaka 1901 H.S.H. Hamoud akivaa nishani kutoka nchi zote mbili za mashariki na magharibi, mwakilishi wa mchango wa kihistoria wa Zanzibar kama mahala pa kukutania kwa wasafiri kutoka katika jamii zote mbili za mashariki na magharibi.

Wanamazingaombwe wa Kihindi

Zanzibar ya zamani ilivutia watumbuizaji kutoka pande zote. Wageni mara kwa mara walitoa maoni kwa hawa watumbuizaji, maranyingi kwa mwelekeo mzuri.

Mandhari ya Mji

J. B. Coutinho alitengeneza picha nyingi kutokea kimo cha juu; hii moja yaonesha kwamba hata zaidi ya miaka 100 hapo nyuma jiji lilikuwa limesongamana na nyumba na majengo makubwa zaidi.